1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Barcelona wakabiliwa na wakati mgumu

18 Aprili 2014

Siku nane tu zilizopita, Lionel Messi na wenzake walikuwa katika nusu fainali ya Champions League, pointi moja nyuma ya Atletico Madrid katika La Liga, na ikijiandaa kwa fainali ya Kombe la Mfalme dhidi ya Real Madrid

https://p.dw.com/p/1BkoA
Fußball King's Cup Finale Real Madrid FC Barcelona
Picha: Javier Soriano/AFP/Getty Images

Sio kawaida kwamba timu kubwa ya soka Ulaya husambaratika haraka sana, kama vile Barcelona ilivyofanya wiki hii. Ni kweli, ulikuwa msimu mgumu kwa Barca, Tito Vilanova kujiuzulu mwezi Julai kama kocha kutokana na saratani ya koo, rais wa klabu Sandro Rosell kujiuzulu Januari kutokana na kashifa ya usajili wa Neymar. Lakini shida hizi zingewekwa kando angalau washinde taji hata moja au mawili hali ambayo ingeipa klabu hiyo utulivu.

Lakini kikosi hicho cha kocha Gerardo Martino kimechimba chini katika wakati mbaya huku safu ya ulinzi ikikabiliwa na majeruhi chungu nzima, nayo ya kiungo ikiyumbayumba, nayo mashambulizi ya ushirikiano wa Neymar na Messi yakiwa butu na yanayotabirika.

Kocha wa Barca Tata Martino amekabiliwa na wakati mgumu tangu alipochukua usukani Camp Nou
Kocha wa Barca Tata Martino amekabiliwa na wakati mgumu tangu alipochukua usukani Camp NouPicha: Getty Images

Barca walibanduliwa nje ya Champions League kwa kushindwa na Atletico Madrid, na sasa wako nyuma ya viongozi hao Atletico katika nafasi ya tatu kwenye la liga, jambo ambalo linafanya iwe vigumu kwa vijana hao kutetea taji hilo.

Na kukamilisha wiki yenye masaibu, barca walifungwa na Real Madrid magoli mawili kwa moja dhidi ya Real MADRID katika fainali ya Kombe la Mfalme. Nini kinachofuata?

Wengi bila shaka wanataka mageuzi makubwa katika kikosi hicho kuanzia kwa kocha. Kwa mujibu wa vyomb vya habari majina yanayopigiwa upatu kuchukua ungozi wa Camp Nou ni kocha wa Borussia Dortmund Jurgen Klopp. Hayo bila shaka tutasubiri kuona namna yatakavyokwenda.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Yusuf Saumu