1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Barua pepe,Mageuzi ya Martin Luther Magazetini

1 Novemba 2016

Kasheshe ya barua pepe za mgombea wa chama cha Democrat cha Marekani Hillary Clinton,Rais wa Uturuki Erdogan na visa vyake dhidi ya wanaomkosoa na miaka 500 tangu Martin Luther alipopendekeza mageuzi ya kanisa Magazetini

https://p.dw.com/p/2RyWe
Deutschland Eröffnung des Lutherjahres 2017 in Berlin
Picha: picture-alliance/dpa/J. Schlueter

Tuanzie lakini Marekani ambako kasheshe mpya ya barua pepe za aliyekuwa waziri wa mambo ya nchi za nje,Hillary Clinton, inazusha wasi wasi miongoni mwa wafuasi wa mgombea huyo wa  kiti cha rais kutoka chama cha Democrats. Gazeti la "Märkische Oderzeitung" linaandika: "Tangazo la Shirika la ujasusi la Marekani FBI kuanza upya uchunguzi wa kile kinachojulikana kama "kasheshe ya barua pepe",ni balaa kwa Hillary Clinton. Kisa hicho kina uma,ingawa bado si dhahir kama kuna kashfa nyuma yake au kama ni mbinu tu za kutaka kumkosesha mgombea huyo wa chama cha Democrat imani ya wapiga kura. Kwasababu hapo hasa ndipo kinapokutikana kishindo. Kwasababu si peke yao wapinzani wake wanaomwangalia Clinton kuwa si mtu wa kuaminika,mwenye kujitafutia masilahi ya kibinafsi na fisadi. Hata hivyo dhidi ya Donald Trump atashinda tu. Mbaya zaidi itakuwa kama kasheshe hiyo ya barua pepe itagubika mhula wa Clinton kama rais."

Wademocrats wasitafute kisingizio

Gazeti la "Fränkische Tag" linatahadharisha dhidi ya kunyoshewa kidole watu wengine. Gazeti linaendelea kuandika: "Wademocrats wasimtupie makosa ya balaa hili jipya James Comey. Ili kuyanusuru mazingira ya kisiasa yasichafuliwe,kiongozi huyo wa FBI anabidi atangaze yaliyomo katika uchunguzi mpya. Akifanya hivyo baada ya uchaguzi,atajiharibia mwenyewe pamoja pia na kuitumbukiza Marekani katika mzozo wa kisiasa. Mgombea anaeshindwa kueleza risala ipi inakutikana katika Computor gani,hajapoteza kitu ikulu ya Marekani. Na kama ndio basi mshindani wake asingebidi kuwa Donald Trump.

Erdogan anapima anaweza kwenda umbali gani

Uturuki inagonga kwa mara nyengine tena vichwa vya habari vya magazeti ya Ujerumani. Rais Reccep Tayyip Erdogan anafanya makusudi,linaandika gazeti la "Mannheimer Morgen":"Erdogan kwa kuanzisha wimbi hili jipya la ukandamizaji dhidi ya vyombo vya habari vinavyomkosoa,pamoja pia na wito wake wa kuanza tena kutumika adhabu ya kifo,anataka  pengine kupima umbali gani anaweza kwenda. Anajua fika: Umoja wa Ulaya unamhitaji katika kukabiliana na mzozo wa wakimbizi. Na hilo ni kweli. Lakini asipatiwe uhuru wa kufanya akitakacho rais huyo wa Uturuki anaezidi kuchukua sura ya muimla. Umoja wa Ulaya ulioiwekea Urusi vikwazo,unabidi uwe na moyoy wa kutumia silaha hiyo hiyo dhidi ya Uturuki pia."

Miaka 500 ya Mageuzi ya Martin Luther

 Ripoti yetu ya mwisho inatujumuisha na wale wanaoadhimisha miaka 500 tangu Martin Luther alipotoa mapendekezo ya kuufanyia marekebisho mwongozo wa kanisa. Gazeti la "Lübecker Nachrichtren" linaandika: "Papa Francis amejiunga na wale wanaomkumbuka mchamungu wa kiinjili, na mwanamageuzi Martin Luther. Ni tukio la aina pekee ambalo ulimwengu haujawahi kushuhudia. Kwa kufanya hivyo Papa Francis ametoa  ishara. Anasogeza mambo mbele,anabadilisha mambo katika uhusiano kati ya wakatoliki na waprotestanti. Lakini hatua zaidi zinabidi zifuate pia. Wanahitaji kusubiri kwa muda gani walioko Vatikan hadi watakapokutana na kupokea sakramenti?

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri:Yusuf Saumu