1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BASRA: Majeshi ya Uingereza yapambana na wanamgambo

26 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBy0

Ripoti zinasema mashambulizi ya majeshi ya Uingereza katika mji wa Basra,kusini mwa Iraq yameua raia wanane.Wakati wa usiku,mjini Basra wanamgambo walishambulia vituo vya majeshi ya Uingereza na Iraq kwa zaidi ya saa mbili wakitumia silaha ndogo ndogo pamoja na mizinga na gruneti zilizorushwa kwa roketi.Mashambulizi hayo yalitokea hiyo jana,saa chache baada ya vikosi maalum vya Iraq mjini humo,kumuua Abu Qader aliekuwa kamanda wa kundi liitwalo “Jeshi la Mehdi” ambalo huongozwa na Shehe wa Kishia, Moqtada al-Sadr.Baadae,al-Sadr ambae tangu mwezi Oktoba mwaka jana,alikuwa mafichoni,alijitokeza msikitini katika mji wa Kufa.Kwa mara nyingine tena,alikariri wito wake wa kutaka majeshi ya kigeni yaondoke Iraq.