1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BASRA:Jeshi la Mahdi kusimamia kituo cha polisi

26 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBVh

Wapiganaji wa Kishia wa Jeshi la Mahdi wanasimamia kituo cha pamoja cha polisi mjini Basra baada ya wanajeshi wa Uingereza kujiondoa na kukabidhi usimamizi kwa polisi wa Iraq.Polisi waliondoka kwenye jingo hilo pale wapiganaji walio wafuasi wa kiongozi wa kidini Moqtada al Sadr anayepinga Marekani walipowasili.

Idadi ndogo ya majeshi ya Uingereza yalisimamia kituo hicho ili kusaidia kutoa mafunzo kwa polisi wa Iraq kabla kujiondoa jana usiku kulingana na makubaliano ya mpango wa kurejeshea Iraq umiliki wa mji.Hayo ni kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Uingereza Mathew Bird.Uingereza imeondoa mamia ya majeshi yake nchini Iraq na kwa sasa alfu 5500 wamesalia kwenye maeneo yaliyo nje ya mji wa Basra.

Wakati huohuo maelfu ya mahujaji wa Kishia wamewasili mjini Karbala hii leo ili kuadhimisha kuzaliwa kwa Imam mmoja aliyepotea katika karne ya 9.Zaidi ya waumini milioni moja wa Kishia kutoka kote ulimwenguni wanatarajiwa kukutana kwenye mji huo tukufu kwa sherehe hizo zinazofikia kilelekesho kutwa jioni na asubuhi Jumatano.Tamasha la Shabaniya zinaadhimisha kuzaliwa kwa Mohamed al Mahdi,Imam wa 12 wa Kishia na wa mwisho aliyetoweka katika karne ya 9.Kulingana na imani ya Kishia Imam huyo alinusurika kifo na atarejea Ulimwenguni ili kudumisha amani na sheria.

Waziri mkuu wa Iraq Nuri al Maliki anawashtumu wanasiasa wa Marekani wanaotoa wito wa kuondoka madarakani na kudai Ufaransa kumuomba msamaha kwa kuchagiza hilo. Kauli hiyo inatolewa baada ya maseneta wawili wa Marekani Carl Levin na mgombea wa Rais Hillary Clinton kutoa wito kwa wabunge wa Iraq kumteua kiongozi mwengine atakayetia kasi juhudi za maridhiano ya kitaifa.