1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern kukwaruzana na Leipzig

Bruce Amani
19 Desemba 2016

RB Leipzig watataka kuukamilisha mwaka wa kushangaza kwa kupata ushindi dhidi ya mabingwa Bayern Munich wakilenga kunyakua nafasi ya kwanza katika msimamo wa Bundesliga kabla ya kuanza mapumziko ya msimu wa baridi

https://p.dw.com/p/2UXBJ
Deutschland Darmstadt 98 gegen FC Bayern München
Picha: imago/J. Huebner

Kama tu Bayern, Leipzig wameshinda 11 kati ya mechi zao 15, wakatoka sare tatu na kupoteza mechi moja. Timu zite zina pointi 36, lakini Bayern wako juu kwa tofauti ya mabao.

Wakati Leipzig walionekana kutamba mwishoni mwa wiki kwa kuwanyamazisha Hertha Berlin mabao mawili kwa sifuri, Bayern walikuwa na kazi ngumu katika ushindi wao wa moja bila dhidi ya Darmstadt.

Hoffenheim timu pekee katika Bundesliga ambayo haijapoteza mchuano wowote kufikia sasa, inashikilia nafasi ya tatu baada ya sare ya 2-2 na Borussia Dortmund. Ina pointi 27 sawa na Hertha ambao ni wa nne. Wolfsburg ilipata ushindi wa bao moja kwa sifuri dhidi ya Eintracht Frankfurt ambao walishindwa kusawazisha kupitia penalti. Sasa Eintracht wanashikilia nafasi ya sita pointi 26 sawa na Dortmund katika nafasi ya tano. Hapo kesho Borussia Dortmund itaikaribisha Augsburg, Borussia Moenchengladbach itacheza dhidi ya VfL Wolfsburg, itakuwa nyumbani dhidi ya Hamburg v Schalke wakati E. Frankfurt watakwaruzana na Mainz

Siku ya jumatano, Hertha Berlin watakuwa wenyeji wa Darmstadt, Cologne watapiga dhidi ya Bayer Leverkusen, Ingolstadt wataangushana na Freiburg, Hoffenheim watafunga kazi dhidi ya Werder Bremen

Mwandishi: Bruce Amani/AP/Reuters/AFP
Mhariri: Iddi Ssessanga