1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAYERN MUNICH

Ramadhan Ali25 Julai 2007

Bayern Munich ndio iliochukua ubingwa mara nyingi kabisa katika Bundesliga-Ligi ya Ujerumani.Msimu uliopita lakini imevuliwa taji na VFB Stuttgart na imeangukia nafasi ya 4 ya ngazi ya Ligi.Itacheza katika kombe la UEFA tu la Ulaya na sio champions League kama desturi yake.

https://p.dw.com/p/CHbb

Franz Beckenbauer,akiwa chipukizi wa miaka 13 alipigwa kibao na mchezaji adui wa klabu ya Münich 1860.

Hii ilimuudhi sana Beckenbauer na badala ya kujiunga mwishoni mwa 1950 na Münich 1860 iliokua ikitamba zaidi wakati ule kuliko Bayern Munich, Franz aliamua kujiunga na FC Bayern.Na hapo akajenga msingi wa kuja kutamba baadae kwa klabu hii na sio tu nyumbani bali hata barani Ulaya.

Beckenbauer,alipanda daraja ya kwanza na Bayern Munich na 1966,Beckenbauer alitwaa taji lake la kwanza la ubingwa.lilikuwa la kombe la shirikisho la dimba la Ujerumani.Ushindi huu ukafuatiwa na wa kombe la washindi la ulaya pale Munich mai 31,1967 ilipoikomea Celtic Glasgow ya Scotland bao 1:0 na kutoroka na kombe.

“Zimebaki dakika 12 kuchezwa katika kipindi cha kurefushwa na matokeo ni bila kwa bila.Roth apiga mkwaju wa freekick,lakini anasitasita kidogo,labda anauweka mpira mbali sana kuliko anapostahiki kupiga.La,aweeza kuupiga.Goal,goal,mpira umeingia langoni.”

Nae Becke nbauer akasema:

“Bulle alikuwa mwepesi zaidi kuliko mlinzi wa waskochi.Na pale akirudi nyuma aliutandika mpira na ukampita kipa wa waskochi.”

Ubingwa wa kwanza wa kimataifa kwea Bayern munich ukawa huo miaka 40 iliopita.Tangu enzi hizo,bayern Munich imefanya mengi:Imeibuka mara tatu klabu bingwa ya Ulaya,bingwa wa dunia wa klabu bingwa,washindi wa kombe la ulaya la UEFA –kombe ambalo watashiriki msimu mpya.

Kuanzia 1974 hadi 1976,hakuna timu iliovuma sana Ulaya kama bayern Munich.kwani,ilitwaa mara 3 mfululizo kombe la klabu bingwa barani Ulaya-leo champions League.Mastadi wake maarufu enzi hizo ni akina kipa Maier,mshambulizi Gerd Müller,Paul Breitner,wingi Uli Hoeness,mlinzi Schwarzenbeck na bila ya shaka nahodha wao Franz Beckenbauer.

Wote hao ni wachezaji wa Bavaria sio kama leo ambapo Bayern Munich ina mchanganyiko wa wachezaji wengi sana wa kigeni.

Kurekodi nyimbo zama zile ilibidi uwe na sauti nzuri.Na Beckenbauer,hakuwa na sauti nzuri hatahivyo, alikuwa stadi wa kwanza mkubwa wa dimba nchini Ujerumani alietembezwa mno na kuuzwa sokoni.

Pale Beckenbauer alipoiacha mkono B.Munich kujiunga na Pele katika Cosmos New York,Bayern munich ilianza kuyumbayumba kidogo na hata kifedha FC Bayern ilianza kuchechemea.

Lakini, Uli Hoeness,akiwa na umri wa miaka 27 wakati ule na ambae aliacha kucheza dimba baada ya kuumia mara kwa mara,akageuka meneja na kuikomboa Munich .Alifaulu kuijenga Bayern munich kuwa miongoni mwa timu bora za ulaya.

“Nilishika dhamana ili kuigeuza Bayern Munich kutoka klabu ya dimba iwe pia kampuni na isiwe inategemea hali ya hewa mara hivi mara vile.Na tulifanikiwa.”

Ili kuwa na kampuni kubwa na imara,unahitaji kuwa na fedha na bila shaka mbinu bora za kutamba sokoni.Na meneja Hoeness alikuwa na werevu huo.Ama huropokwa binafsi au akishindwa huwaajiri wenye kujua zaidi kusema.Alimuajiri kocha wa kitaliana Giovanni Trapattoni:

4.O-Ton Trapattoni:

“Je,Kocha ni mpumbavu.Kocha anajua kinapita nini uwanjani.Kuna wachezaji,wawili,watatu hivi wanacheza kama chupa tupu isio na kitu.”

Kocha Trapattoni.bayern Munich ikazidi kutajirika na kutawazwa mabingwa wa ujerumani mara kadhaa ikiwa ni rekodi.

Ndoto yake kubwa ilionesha kana kwamba haingetimilia-yaani kutwaa champions _league-kombe la sasa la klabu bingwa barani ulaya:

Mei,26,1999 ikajipatioa nafasi ya kutwaa kombe hilo ilipokumbana finali mjini Barcelona na Manchester united. Wakati Munich hadi dakika ya mwisho ikihisi imeilaza Manchester kwa bao 1:0,Manchester sio tu ilisawazisha bali ilitia pia bao la ushindi la Cunnigham na kuinyima B.munich kombe la champions League.

Mei 23,2001,Mumnich ikacheza tena finali ya champions League na baada ya kurefushwa mchezo Munich na Valencia zilisimama sare bao 1:1.Mikwaju ya adhabu ya penalty.

“Sasa Pelegrino amerudi nyuma masafa marefu na anakwenda mbele kupiga penalty.Oliver Kahn aizuwia na Bayern Munich imelitwaa kombe la klabu bingwa.Kahn anyanyua mikono juu na Bayern Munich ni mabingwa wa champions League”.