1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern wadondosha pointi kileleni

3 Desemba 2012

Sasa tutupie jicho ligi ya soka hapa Ujerumani Bundesliga ambapo uongozi wa ligi wa Bayern Munich umepunguzwa hadi point nane nyumbani na mabingwa watetezi Borussia Dortmund

https://p.dw.com/p/16uxH
Fußball Bundesliga 15. Spieltag: FC Bayern München - Borussia Dortmund am 01.12.2012 in der Allianz Arena in München (Bayern). Bayerns Javier Martinez (l) im Kampf um den Ball mit Mario Götze aus Dortmund. Foto: Marc Müller/dpa (Achtung: Hinweis zur Bildnutzung! Die DFL erlaubt die Weiterverwertung von maximal 15 Fotos (keine Sequenzbilder und keine videoähnlichen Fotostrecken) während des Spiels (einschließlich Halbzeit) aus dem Stadion und/oder vom Spiel im Internet und in Online-Medien. Uneingeschränkt gestattet ist die Weiterleitung digitalisierter Aufnahmen bereits während des Spiels ausschließlich zur internen redaktionellen Bearbeitung (z.B. via Bilddatenbanken).) +++(c) dpa - Bildfunk+++
FC Bayern München vs. Borussia DortmundPicha: picture-alliance/dpa

Huyo ulikuwa ni mchuano wa sita mfululizo kwa Bayern kushindwa kuwapiku mahasimu hao. Bayer Leverkusen nao wanaendelea kuishikilia nafasi ya pili baada ya kupata ushindi wa goli moja kwa sifuri dhidi ya Nuremberg ikiwa ndio ushindi wao wa sita katika mechi saba. Leverkusen wako katika nafasi ya pili na pointi 30 huku Dortmund wakiwa katika nafasi ya tatu na pointi 27, pointi mbili mbele ya Schalke 04 ambao walitoka sare ya kufungana bao moja kwa moja na Borussia Moenchengladbach.

Hoffenheim yamtimua Markus Babbel

Naye mkufunzi Markus Babbel amelazimika kufunganya virago baada ya Hoffenheim kuwazabwa na Werder Bremen magoli manne kwa moja na kumwongezea shinikizo mkufunzi huyo. Hicho kilikuwa kichapo cha nne mfululizo na Hoffenheim bado wako katika nafasi ya kushushwa daraja. Augsburg nao walitoshana nguvu na Freiburg kwa kufungana goli moja kwa moja. Huyu hapa kocha Markus Weinzierl

Markus Babbel ametimuliwa kama mkufunzi wa Hoffenheim
Markus Babbel ametimuliwa kama mkufunzi wa HoffenheimPicha: picture-alliance/dpa

Wakati huo huo, Beki wa katikati wa Bayern Munich Holger Badstuber amefanyiwa upasuaji leo baada ya kupata jeraha la msuli katika goti lake la kulia. Badstuber sasa atakuwa nje kwa miezi mitano. Mlinzi huyo aliyekuwa amerejea tu uwanjani baada y akuwa nje kwa wiki tatu kutokana na jeraha, aliumia goti la kulia baada ya kukabiliana na mchezaji mwenzake wa Ujerumani Mario Goetze wakati wa mchuano wa mwishoni mwa wiki waliotoka sare ya goli moja kwa moja na Dortmund.

Kule Ungereza, Manchester United ilisonga mbele kwa tofauti ya pointi tatu kileleni mwa Premier League baada ya mchuano wa kusisimua uliokamalika kwa ushindi wa magoli manne kwa matatu dhidi ya Reading wakati Mabingwa watetezi Manchester City wakitekwa kwa sare ya kufungana goli moja kwa moja na Everton. Kaimu mkufunzi wa Chelsea Rafael Benitez alishuhudia timu yake ikifungwa magoli matatu licha kuwa ilikuwa ikiongoza kwa goli moja kwa sifuri katika kipindi cha kwanza. Arsenal waliteremka hadi nafasi ya kumi baada ya kuduwazwa nyumbani na Swansea magoli mawili kwa sifuri. United wanaongoza msururu na pointi 36 wakijianda akwa mchuano wa wikendi ijayo dhidi ya Manchester City ambao wako katika nafasi ya pili na pointi 33. Chelsea ni wa tatu na pointi 33 sawa na Tottenham Hotspur, na Westbrom Albion.

Ligi ya Mabingwa: 16 za mwisho

Vilabu sita vinashiriki michuano ya Ligi ya Mbaingwa barani Ulaya, UEFA Champions League wiki hii vikiwa na matumaini ya kupata mojawapo ya nafasi tatu za 16 za mwisho ambazo bado ziko wazi. Hata hivyo hatima ya mabingwa watetezi Chelsea haiko mikononi mwao kabisa. Chelsea wanang'ang'ana na Juventus kwa nafasi ya pili katika kundi E lakini hata kama watawashinda Nordsjaelland katika uga wa Stamford Bridge siku ya Jumatano watakuwa mabingwa wa kwanza kuondolewa katika awamu ya makundi kama Juve wataepuka kichapo dhidi ya Shaktar Donetsk.

Nembo ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, UEFA Champions League
Nembo ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, UEFA Champions League

Celtic na Benfica bado wana nafasi y akujiunga na mabingwa wa kundi C Barcelona katika awamu ya maondowano wakati Galatasaray au CFR Cluj wakimaliza katika kundi G kama nambari mbili. Kwa timu nyingine ambazo tayari zina nafasi katika droo ya kumi na sita za mwisho mnamo Desemba 10, mechi zao za mwisho zitaamua kama zitafuzu kama washindi wa makundi yao.

Hata wale ambao hawana nafasi ya kufuzu watalenga kujiliwaza na zawadi ya kushiriki katika dimba la pili la Europa League. Celtic watakutana na Spartak Moscow Jumatano, wakati Galatasaray wakiangushana na Braga wakitaraji kuwa Cluj watawazidi guvu Manchester United uwanjani Old Trafford. Jumanne Paris St Germain watalenga kuwazidi nguvu Porto mjini Paris katika kundi A. Bayern pia watamaliza kama washindi wa kundi F mbele ya Valencia kama watasajili ushindi dhidi ya BATE Borisov Jumatano. Manchester City watachuana na washindi wa kundi D Borussia Dortmund.

Mwandishi: Bruce Amani/Reuters/DPA/AFP

Mhariri:Yusuf Saumu