1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern yaifunza soka Stuttgart

3 Septemba 2012

Bayern Munich yaisambaratisha VFB Stuttgart mabingwa Borussia Dortmund bado yasua sua,Ronaldo hana raha Real Madrid,na Van Persie aweka wavuni mabao matatu katika ushindi wa Manchester United dhidi ya Southhampton.

https://p.dw.com/p/162nr
Bayern's player's celebrate after scoring during the German first division Bundesliga soccer match between FC Bayern Munich and VFB Stuttgart, in Munich, Germany, Sunday, Sept. 2, 2012. (Foto:Kerstin Joensson/AP/dapd) - NO MOBILE USE UNTIL 2 HOURS AFTER THE MATCH, WEBSITE USERS ARE OBLIGED TO COMPLY WITH DFL-RESTRICTIONS, SEE INSTRUCTIONS FOR DETAILS -
Wachezaji wa FC Bayern wakishangiria moja kati ya mabao yao 6-1 dhidi ya - VfB StuttgartPicha: Getty Images/AFP

Eintracht Frankfurt imeuanza msimu huu wa Bundesliga kwa vishindo. Timu hii iliyopanda daraja msimu huu imepata ushindi wa pili wiki hii baada ya kuicharaza 1899 Hoffenheim kwa mabao 4-0. Hoffenheim kwa upande wake umeonyesha mchezo dhaifu sana katika michezo miwili hadi sasa ya Bundesliga msimu huu na kumaliza mchezo huo ikiwa na wachezaji tisa uwanjani.

Wachezaji Sejad Salihovic na Stephan Schrock walionyeshwa kadi nyekundu katika dakika ya 70 na 73.

Fußball Bundesliga 2. Spieltag: TSG 1899 Hoffenheim - Eintracht Frankfurt am Samstag (01.09.2012) in Sinsheim in der Rhein-Neckar-Arena. Hoffenheims Eren Derdiyok zieht sich sein Trikot über den Kopf. Foto: Uwe Anspach dpa/lsw (Achtung Hinweis zur Bildnutzung! Die DFL erlaubt die Weiterverwertung von maximal 15 Fotos (keine Sequenzbilder und keine videoähnlichen Fotostrecken) während des Spiels (einschließlich Halbzeit) aus dem Stadion und/oder vom Spiel im Internet und in Online-Medien. Uneingeschränkt gestattet ist die Weiterleitung digitalisierter Aufnahmen bereits während des Spiels ausschließlich zur internen redaktionellen Bearbeitung (z. B. via Bilddatenbanken).) +++(c) dpa - Bildfunk+++
Ni aibu mchezaji wa 1899 Hoffenheim -Eren Derdiyok akionekana kusema baada ya mchezo na Eintracht FrankfurtPicha: picture alliance / dpa

Borussia Moenchengladbach waliridhika na sare ya bila kufungana na majirani zao wa Fortuna Dusseldorf , licha ya Moenchengladbach kutawala mchezo kwa kipindi kirefu.

Borussia Dortmund mabingwa watetezi wa Bundesliga walishindwa pia kuvunja ukuta mgumu wa FC Nürnberg, ambao walicheza kwa tahadhari kubwa wakilinda lango lao kwa umakini. Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.

Fußball Bundesliga 2. Spieltag : 1. FC Nürnberg - Borussia Dortmund am Samstag (01.09.2012) im easyCredit-Stadion in Nürnberg (Mittelfranken). Pekhart von Nuernberg (nicht im Bild) erzielt das 1:0 gegen Torwart Roman Weidenfeller (M) und Ilkay Guendogan (r). Foto: Sven Grundmann dpa/lby (Achtung Hinweis zur Bildnutzung! Die DFL erlaubt die Weiterverwertung von maximal 15 Fotos (keine Sequenzbilder und keine videoähnlichen Fotostrecken) während des Spiels (einschließlich Halbzeit) aus dem Stadion und/oder vom Spiel im Internet und in Online-Medien. Uneingeschränkt gestattet ist die Weiterleitung digitalisierter Aufnahmen bereits während des Spiels ausschließlich zur internen redaktionellen Bearbeitung (z.B. via Bilddatenbanken).) +++(c) dpa - Bildfunk+++
1. FC Nürnberg - waliwawekea ngumu Borussia DortmundPicha: picture alliance / dpa

Werder Bremen ilifanikiwa kupata points zote tatu dhidi ya SV Hamburg , baada ya ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa watani wa jadi wa eneo la kaskazini mwa Ujerumani.

Lakini kipigo cha mbwa mwizi kiliwaangukia VFB Stuttgart nyumbani kwa Bayern Munich, ambapo Bayern ilipata karamu ya magoli 6-1. Ushindi huo haukutarajiwa dhidi ya timu hiyo ambayo imeonesha mabadiliko makubwa msimu uliopita chini ya kocha Bruno Labadia.

Lakini hadi mapunziko, Bayern ilikuwa inaongoza kwa mabao 3-1. Mkurugenzi wa sport wa Stuttgart Fredi Bobic hakuwa na zaidi la kusema ila kukubali yaishe.

"Haikuonyesha tangu mwanzo kuwa tungewapa Bayern nafasi kubwa kiasi hicho katika uwanja wao kuweza kutushambulia kwa kushtukiza, licha ya kuwa tulikuwa tunaongoza kwa bao 1 kwa bila".

Mchezaji wa kiungo wa Bayern Munich Toni Kroos alipoulizwa iwapo Bayern inaonesha ubabe wake katika bundesliga msimu huu baada ya kukosa kupata taji lolote kwa misimu miwili mfululizo, alisema :

"Sijui. Nafikiri Bayern Munich inapaswa kuwa kama ilivyo sasa kila wakati, kwamba upinzani dhidi yetu utakuwapo na wachezaji wapya watakuja . Uwezo huo Bayern inao".

Kipigo cha mabao 4-0 ilichopata VFL Wolfsburg dhidi ya Hannover 96 kimemshangaza hata kocha wao Felix Magath. Timu hiyo ya watengeneza magari ya Volkswagen imetumia kitita cha euro milioni 20 kununua wachezaji wapya msimu huu lakini haikutosha kuweza kuliokoa jahazi la Wolfsburg. Kocha Felix Magath amesema , "sio tu kwamba nimeshangazwa kidogo, lakini nimeshangazwa sana na kipigo hiki. Tulijitayarisha vizuri baada ya mchezo mzuri tulioonesha dhidi ya Stuttgart wiki iliyopita na tulitaka kufanya hivyo tena leo".

Nae mchezaji wa kiungo wa Hannover Sergio da Silva Pinto amesema kwao mambo ni poa kabisa.

"Tumefarijika sana, kwamba tumeweza kushinda na hasa jinsi tulivyopata ushindi huu, kwa kweli inafanya soka kuwa na raha sana".

La Liga nayo

Wakati huo huo Cristiano Ronaldo amepachika mabao mawili na kuhakikisha ushindi wa Real Madrid wa mabao 3-0 dhidi ya Granada katika ligi ya Uhispania La Liga na Barcelona ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Valencia.

Portugal's Cristiano Ronaldo reacts during the Euro 2012 semi-final soccer match against Spain at Donbass Arena in Donetsk, June 27, 2012. REUTERS/Charles Platiau (UKRAINE - Tags: SPORT SOCCER)
Ronaldo hana raha Real MadridPicha: Reuters

Chelsea , ambayo ilipata kipigo cha mabao 4-1 dhidi ya Atletico Madrid katika mchezo wa Super Cup siku ya Ijumaa ilijitutumua katika ligi ya Uingereza , Premier League na kujikusanyia points tisa kutokana na michezo mitatu wakati mabingwa Manchester City, mahasimu wao Manchester United na Arsenal London wote wakipata ushindi mwishoni mwa juma na kupunguza mwanya wa points.

Baada ya michezo mitatu hadi sasa ya Premier League , Chelsea ni timu pekee ikiwa na rekodi ya asilimia 100 ya ushindi baada ya Swasea City kulazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Sunderland na Everton kuangukia pua dhidi ya West Bromwich Albion.

Van Persie aliyetia saini kuitumikia Manchester United kwa kitita cha pauni milioni 24 , akitokea Arsenal aliweka wavuni mpira mara tatu , katika ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Southampton na kufikisha mabao 100 katika premier league.

Na huko Italia

Huko Italia mabingwa Juventus Turin wameshinda mchezo wao wa pili wa ligi ya Italia , Serie A, kwa kuikandika Udinese mabao 4-1 baada ya mlinda mlango wa wenyeji Udinese kutolewa nje kwa kadi nyekundi katika dakika ya 13.

Lazio ambao waliilaza Palermo kwa mabao 3-0 walisaidiwa na mabao mawili ya mshambuliaji wa Ujerumani Miroslav Klose, pamoja na Napoli ambao wameishinda Florentina kwa mabao 2-1 wote wana points sita.

Huko Ufaransa vumbi linatimka

Huko Ufaransa Zlatan Ibrahimovic alipachika wavuni mabao mawili na kuipatia ushindi wa kwanza Paris St Germain katika ligi ya Ufaransa msimu huu dhidi ya Lille, ambapo mchezo huo ulimalizika kwa ushindi wa mabao 2-1 kwa PSG.

Olympique Marseille imeendelea kutamba msimu huu kwa kuishinda Stade Rennes kwa mabao 3-1 na Olympique Lyonnnes ikaishinda Valenciennes kwa mabao 3-2 na kujipachika katika nafasi ya pili ikiwa na points 10 wakati Lorient iko nafasi ya tatu baada ya kuilambisha Nancy mabao 3-0.

Kocha ataka washambuliaji zaidi

Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers anakiri kuwa atalazimika kuingia mkataba na wachezaji walio huru kama Michael Owen na Didier Drogba baada ya klabu yake kuanza vibaya kabisa msimu huu wa Premier League kwa muda wa miaka 50.

Baada ya kumruhusu Andy Carroll kujiunga na West Ham kwa mkopo , Rodgers alitarajia kuwa viongozi wa klabu hiyo kupata saini ya mshambuliaji Clint Dempsey kutoka Fulham. Lakini badala yake mchezaji huyo amehamia Tottenham. Baada ya kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Arsenal jana Jumapili , kocha Rodgers anakabiliwa na matatizo makubwa katika nafasi ya ushambuliaji.

Ronaldo hafurahii maisha Real

Cristiano Ronaldo anataka kuwakimbia mabingwa wa Uhispania Real Madrid kwasababu hana raha katika klabu hiyo, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari leo. Hii ni tafsiri ya magazeti ya AS, Sport na Mundo Desportivo miongoni mwa vyombo vingine vya habari , ambayo imetolewa baada ya matamshi yake ya kushangaza baada ya kupachika mabao wawili katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Granada jana Jumapili na kushindwa kushangiria.

Kombibild Fußballer des Jahres 2012 Ronaldo, Messi, Iniesta
Mchezaji bora wa FIFA mwaka huu 2012 Iniesta akiwa na Ronaldo, na MessiPicha: dapd/Getty Images/DW

Sina raha na watu hapa wanafahamu ni kwa nini, ameongeza Ronaldo. Magazeti ya AS, Sport na Mundo Deportivo yamesema kuwa Ronadlo amemwambia rais wa Real , Florentino Perez siku ya Jumamosi kuwa anataka kuondoka katika klabu hiyo kwasababu Real hawafanyi juhudi kumsaidia kupata tuzo ya mchezaji bora wa dunia wa FIFA, tuzo iliyokwenda kwa mchezaji wa Barcelona Andres Iniesta msimu huu na ambayo Lionel Messi wa Barcelona pia ameshinda mara tatu.

Na katika bara la Afrika

Esperance ya Tunisia imenyakua nafasi ya kwanza katika kundi lake la champions league ya shirikisho la kandanda barani Afrika CAF kwa ushindi wa bao 1-0 nyumbani kwa Sunshine Stars ya Nigeria. Ushindi huo umeendeleza ushindi wa 19 bila kufungwa kwa mabingwa hao wa Tunisia ambao wanawania ubingwa wa pili mfululizo katika bara la Afrika baada ya kuishinda Wydad Casablanca ya Morocco katika fainali mwaka jana.

Etoile Sahel ya Tunisia iliondolewa katika mashindano hayo na shirikisho la kandanda barani Afrika CAF Jumatatu iliyopita baada ya mashabiki wake kuvamia uwanja katika mchezo wa nyumbani dhidi ya Esperance na matokeo yake ya awali yalifutwa.

Esperance itakabiliana sasa na mshindi wa pili wa kundi B katika nusu fainali na Sunshine ambayo ni mshindi wa kundi B pamoja na TP Mazembe ya DRC pamoja na Al Ahly ya Misri zimejihakikishia kusonga mbele lakini zinapaswa kuamua ni timu gani inashika nafasi ya kwanza. Mazembe ina miadi na Berekum Chelsea ya Ghana wakati matokeo tofauti mjini Accra yanaweza kuiruhusu Al Ahly ya Misri kuibuka mshindi wa kwanza katika kundi hilo la B iwapo timu hiyo itaishinda Zamalek mjini Cairo katika pambano la watani wa jadi.

Michezo ya walemavu

Katika michezo ya Paraolympics mjini London, Oscar Pistorius wa Afrika kusini jana alivuliwa taji ambapo mchezaji chipukizi wa Brazil Alan Oliveira alipata ushindi katika mbio za mita 200. Lakini Pistorius mwenye umri wa miaka 25 alisema baada ya kuvuliwa taji hilo kuwa , analalamika kwa kuwa hakuwa na nafasi kwa kuwa wenzake walikuwa na miguu mirefu ya bandia ya kukimbilia.

Eine Frau tanzt am Samstag (11.07.2009) beim International Paraolympic Day 2009 in Berlin mit einem Mann in einem Rollstuhl. Im Hintergrund ist das Brandenburger Tor zu sehen. Foto: Klaus-Dietmar Gabbert dpa/lbn +++(c) dpa - Bildfunk+++
Michezo ya walemavu ya Olympic mjini LondonPicha: picture-alliance/dpa

Lakini mkimbiaji huyo kutoka Afrika kusini ameomba radhi leo kwa matamshi yake hayo , lakini maesisitiza kuwa kuna umuhimu wa kujadiliwa kuhusu miguu mirefu ya bandia ya kukimbilia.

Hadi sasa China inaongoza katika kujikusanyia medali ikiwa na medali 35 za dhahabu , 24 za fedha na 14 za shaba, na jumla ya medali 87.

Uingereza inashika nafasi ya pili ikiwa na jumla ya medali 54 na 14 za dhahabu na Ukraine inashikilia nafasi ya tatu. Ujerumani inashikilia nafasi ya nane ikiwa na dhababu 5, fedha 8 na shaba 8.

Nigeria inaongoza orodha hiyo kwa mataifa ya Afrika ikiwa na dhahabu 4, fedha 4 na haina medali ya shaba. Afrika kusini iko katika nafasi ya 19, Misri ni ya 25 na Tunisia inashika nafasi ya 30.

Kwa taarifa hizo mpenzi msikilizaji ndio tunafikia mwisho wa kuwaletea habari hizi za michezo kwa leo. Hadi mara nyingine jina langu ni Sekione Kitojo nasema kwaherini.

Mwandishi : Sekione Kitojo / afpe / rtre / dpae

Mhariri : Yusuf Saumu