1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern yaingia nusu fainali kuwania ubingwa barani Ulaya

Josephat Nyiro Charo8 Aprili 2010

Mkwaju wa Robben waiokoa Bayern

https://p.dw.com/p/Mpwh
Jogoo wa Bayern Munich Arjen Robben, kushoto, akishangilia bao lake na wachezaji wenzake, Philipp Lahm (katikati) na Mario GomezPicha: AP

Msema kweli amejulikana baada ya miamba ya soka ya timu mbili Manchester United na Bayern Munich kujibwaga uwanjani jana katika awamu ya pili ya robo fainali kwenye michuano ya kuwania taji la mabingwa Barani Ulaya.

Manchester United ilipata bao lake lw kwanza kutoka kwa mkwaju wa Darron Gibson na mabao mengine mawili kutoka kwa mshambulizi wake matata, Nani. Lakini Ivca Olic wa Bayern Munich aliifungia timu yake bao muhimu kabla ya kipindi cha mapumziko, liliyafufua matumaini ya timu kuweza kusonga mbele.

Kipindi cha pili Man U ilimpoteza mchezaji wake Rafael da Silva pale alipoonyeshwa kadi mbili za njano, na hivyo kuiwezesha Bayern kutamba na mpira uwanja mzima na hatimaye Arjen Robben kutiwa wavuni bao la pili nakuyazika matumaini ya vijana wa Alex Furgusson nyumbani kwao Old Trafford.

Jitihada za Bayern kufuzu katika timu nne za mwisho zilipewa nguvu baada ya kurudi mchezaji wao mholanzi Arjen Robben ambaye alisema yupo fiti kushiriki mchuano wa jana baada ya kuukosa ule wa wiki jana kutokana na jeraha la mguu uliopelekea ushindi wao dhidi ya Schalke.

Bayern Munich pia ilimchezesha mchezaji wa kiungo cha kati Bastian Schweinsteiger aliyesimamishwa kucheza kwa muda.

Hata hivyo mchuano wa jana ulitarajiwa kukosa msisimko uliodhihirika katika mchuano wa awamu ya kwanza wa timu ya Munich na Man U kwa wasiwasi wa kukosekana kushiriki kwa jogoo la Man U Wayne Rooney aliyekuwa ameumia mguu katika mchuano uliomalizika na uliopelekea ushindi wa Munich kwa ambao 2-1. Wayne hata hivyo alicheza na kutoa mchango kabla ya kupumzishwa na kocha wake.

Hali ilikuwa sio nzuri kwa Arsenal hapo juzi hata baada ya Bendtner kujizatiti kunako dakika 18 za kwanza kubusu kimia cha Barcelona,mkondo uliwageukia baada ya wao kuzimwa mabao 4-1 na FC Barcelona kufuatia mahanjam ya chipukizi Lionel Messi mwenye umri wa miaka 22 yaliopelekea ushindi wa timu yake kwa kufunga mabao 3 kabla ya kipenga cha kumalizika kwa awamu ya kwanza ya mchuano huo.

Mkufunzi wa timu hiyo ya Barca, Pep Guirdiola alikuwa mwingi wa sifa kwa mchezaji wake akisema hamna maneno ya kumfafanua Messi kwa umahiri wake katika soka.

Amemtaja Messi kama mfano mwema kwa wachezaji wengine chipukizi katika soka lakini anasema hatahivyo ni vigumu mno kwa yeyote kumuiga.

Guirdiola vile vile aliwasifu wachezaji wake wengine ambao anasema anafahamu hawatomulikwa kwenye vyombo vya habari lakini anasema wanaitambisha timu ya Barca kutokana na mchezo wao mzuri.

Hali ilivyo kwa timu tajiri ya Arsenal sio nzuri kwa muda wa misimu mitano mfululizo na ambapo imeshindwa kunyakua taji lolote.

Ni mpaka vijana wa Wenger watakapojizatiti na kujaribu kuwashinda wana wa 'The blues' yaani Chelsea na mahasimu wengine Man U katika hatua za mwisho za ligi kuu ya England Premier League ndipo mambo yatakapowaendea sawa la sivyo msimu huu pia utakwisha bila ya wao kunyakua taji lolote.

Kushindwa kwao hapo jana na timu ya Barca kumewatoa Arsenal katika mashindano ya kombe hilo la Champions League.

Ushindi wa mwisho kwa Arsenal ulikuwa mnamo mwaka 2005 waliponyakua kombe la FA.

Tangu hapo wakati huo Wenger ameipangua timu yake akiwajumuisha vijana bado lakini bahati haijawaangukia.

Mwandishi :Maryam Abdalla/RTRE

Mhariri:Mohammed Abdulrahman