1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING: 25 wauwawa katika mlipuko

5 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBlg

Watu 25 wameuwawa na wengine 33 wamejeruhiwa kufuatia mlipuko ndani ya klabu ya starehe mjini Tianshifu katika mkoa wa Liaoning ulio kaskazini mashariki mwa China.

Shrika la habari la Xinhua limesema kuwa kilichosababisha mlipuko huo bado hakijajulikana.

China imekumbwa na mfululizo wa mioto na ajali zinginezo katika maeneo ya umma licha ya serikali kuahidi kuwa itaimarisha usalama.

Ajali nyingi zimehusishwa na kutofuatwa tahadhari za kiusalama.