1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING: China imeahidi kuongeza misaada yake barani Afrika

5 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCvw

China katika mkutano wa siku mbili kati ya nchi hiyo na madola ya Kiafrika mjini Beijing,imeahidi kutoa mabilioni ya Dola kuzisaidia nchi za Kiafrika.Rais Hu Jintao wa China,amesema nchi yake itatoa mikopo ya Dola bilioni 5 na itaongeza maradufu msaada wake kwa bara Afrika hadi mwaka 2009.Miradi ya kutoa mafunzo kwa vijana 15,000 wa Kiafrika itaanzishwa.Maafisa wa China wamesema, wanapanga kujenga shule,hospitali na zahanati za kupambana na malaria sehemu mbali mbali za bara Afrika.Mkutano wa Beijing ni mkutano mkubwa kabisa wa kilele kupata kufanywa kati ya China na Afrika,ukihudhuriwa na viongozi 48 kutoka nchi 53 za Kiafrika.