1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING: China itaongeza matumizi ya majeshi yake

4 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCMX

China inatazamia kuongeza matumizi yake ya kijeshi kwa takriban asilia 18.Msemaji wa Baraza la Kitaifa la Umma alitoa taarifa hiyo katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Beijing. Jiang Enzhu amesema,kiasi ya kama Euro bilioni 34 zitahitajiwahi ili kuweza kulifanya jeshi kuwa la kisasa.Akaongezea kuwa azma ya mkakati wa ulinzi, ni kuhifadhi usalama na muungano wa kitaifa. Tangazo hilo limetolewa siku moja baada ya China kueleza upinzani wake kuhusu mpango wa Marekani wa kutaka kuiuzia Taiwan makombora 450 ya angani na ardhi kavu.Serikali ya Beijing huitazama Taiwan kama ni jimbo lake lililoasi.