1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beijing. China kutoa misaada zaidi kwa Afrika.

4 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCwA

China imesema mwanzoni mwa mkutano wa nchi hiyo na mataifa ya Afrika kuwa inataka kufanya zaidi katika muda wa miaka mitatu ijayo kusukuma mbele maendeleo katika bara la Afrika.

Rais Hu Jintao amesema kuwa nchi yake itatoa mikopo na misaada yenye thamani ya dola bilioni 5, na kuongeza mara dufu msaada wake kwa Afrika hadi ifikapo 2009.

Mipango ya mafunzo kwa vijana 15,000 itafanyika na maafisa wa China wanasema kuwa wanapanga kujenga shule, hospitali na zahanati za kupambana na malaria sehemu mbali mbali katika bara la Afrika.

China ina matumaini ya kuimarisha uhusiano wake katika bara hilo lenye maliasili nyingi.