1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING: Kampuni ya China yanunua uwanja wa ndege Ulaya

26 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CByK

Kwa mara ya kwanza wawekezaji wa China wamenunua uwanja wa ndege barani Ulaya.

Kampuni ya LinkGlobal imelipa kiasi Euro milioni mia moja kununua uwanja mdogo wa ndege wa Parchim ulio kati ya Berlin na Hamburg, kaskazini mwa Ujerumani.

Uwanja huo wenye upana wa kilomita tatu unakarabatiwa ili kuhudumia ndege za uchukuzi wa mizigo baina ya Ujerumani na China.

Kufikia mwakani, uwanja huo unatarajiwa kuhudumia ndege tano za mizigo kila siku.

Wakati huo huo Rais wa Ujerumani, Horst Köhler amekutana na Waziri Mkuu wa China, Wen Jia Bao mjini Beijing ambapo aliisifu China kwa kuuimarisha uchumi wake.

Rais Horst Köhler amesema Ujerumani pia inafaidika na harakati hizo za China na kwamba uhusiano wa kiuchumi kati ya mataifa hayo mawili ni mzuri.

Hata hivyo Rais Horst Köhler alisema masuala ya haki za kibinadamu nchini China hayajazingatiwa ipasavyo.

Rais huyo wa Ujerumani pia alisema China imeweka viwango vya hali ya juu vya kutunza mazingira na kwamba nchi hiyo inataka kufaidika kiufundi kutoka Ujerumani.