1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING: Kimbunga SEPAT kimefika barani China.

19 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBXk

Watu wawili wameuawa katika maporomoko ya ardhi kwenye Wilaya ya Fuji na 9 wengine waliuawa katika kimbunga kilichotokea wilaya ya jirani ya Zhejiang.Maafisa nchini China wametangaza hali ya tahadhari.Kiasi ya watu milioni moja wanaoishi sehemu za pwani wamehamishwa kwengine.Kwa mujibu wa takwimu za hivi sasa,katika mwezi wa Julai peke yake,watu 712 wameuawa katika vimbunga na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha.Watu 163 bado hawajulikani walipo.