1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beijing. Korea ya kaskazini yakubali ili yaishe.

20 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD0j

Kiongozi wa Korea ya kaskazini Kim Jong Il amemwambia mjumbe maalum wa China aliyemtembelea kuwa nchi hiyo haina mpango wa kufanya jaribio la pili la silaha za kinuklia .

Kim alitoa maelezo hayo mjini Pyongyang jana Alhamis wakati wa mazungumzo na mjumbe wa China Tang Jiaxuan.

Wizara ya mambo ya kigeni ya Japan imesema kuwa haiwezi kuthibitisha ama kupinga ripoti hiyo, ambayo imekuja wakati waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice akiwa mjini Beijing kutafuta kuungwa mkono kwa vikwazo vya umoja wa mataifa dhidi ya Korea ya kaskazini kutokana na kufanya jaribio la silaha za kinuklia hapo Oktoba 9.

Rice amesema kuwa Tang ametoa ujumbe mkali kwa Wakorea ya kaskazini na kuweka wazi kwao kuwa China itatekeleza kwa ukamilifu vikwazo vya umoja wa mataifa.

Waziri wa mambo ya kigeni wa China Li Zhaoxing amesema kuwa Tang na viongozi wa Korea ya kaskazini wamezungumzia pia jinsi ya kuanzisha tena mazungumzo ya nchi sita yaliyokwama kuhusu mpango wa kinuklia wa nchi hiyo.