BEIJING: Mazungumzo ya mataifa sita yashindwa kufua dafu
22 Desemba 2006Matangazo
Mazungumzo ya mataifa sita kuhusu mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini yamemalizika leo mjini Beijing China pasipo makubaliano kufikiwa. Shirika la habari la Korea Kusini limeripoti kwamba hakuna tarehe nyengine ya mazungumzo iliyopangwa.
China iliyoyaandaa mazungumzo hayo imesema lengo kubwa lilikuwa kulifanya eneo la Korea kuwa huru kutokana na silaha hizo. Mazungumzo hayo yalianza Jumatatu wiki hii baada ya kukwama kwa miezi 13.
Serikali ya Pyongyang imeitaka Marekani iondoe vikwazo vyake vya kifedha dhidi yake pamoja na kufunguliwa kwa akaunti za benki zilizofungiwa. Korea Kaskazini ilifanya majaribio ya zana zake za kinyuklia mnamo Oktoba 9 mwaka huu.