1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beijing: Waziri mkuu wa Israel ziarani Uchina.

9 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CBHl

Waziri mkuu wa Israel, Ehud Olmert, amewasili Uchina kwa ziara yenye lengo la kuimarisha maingiliano ya kiuchumi, kiteknolojia na kijeshi baina ya nchi hizo mbili. Bwana Olmert pia anatazamiwa kuzungumzia juu ya mpango wa kinyukliya wa Iran wakati wa ziara hiyo ya siiku tatu, na ambayo itaingiza pia mazungumzo na waziri mkuu Jiabo, na waziri wa biashara, Bao Xilai. Ziara hiyo inasadifu na maadhimisho ya miaka 15 ya uhusiano wa kibalozi baina ya nchi hizo mbili.