1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING: Waziri mkuu wa Urussi ziarani China

9 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCuV

China na Urussi zimekubaliana kupanua uhusiano wao wa kibiashara,hasa kushirikiana katika sekta nishati.Waziri mkuu wa Urussi Michail Fradov amewasili Beijing leo hii kwa ziara ya siku mbili.Wakati huo,anatazamiwa kutia saini mikataba 17 ya biashara ikiwa ni pamoja na makubaliano ya uwekezaji na mambo ya benki na juu ya usimamizi wa mipaka.Urussi inataka kuongeza idadi ya mafuta inayosafirishwa China kwa njia ya reli kufikia tani milioni 15 katika kipindi cha mwaka huu.Nchi hizo mbili pia zimepanga kutumia Dola bilioni 10 katika muda wa miaka mitano ijayo kujenga vinu vya nishati kando ya mipaka yao ili kutekeleza mahitaji ya nishati yanayozidi kuongezeka nchini China.