1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING:China yapinga vikwazo vipya dhidi ya Iran

30 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7BJ

China imesema kwamba vikwazo vipya dhidi ya Tehran visitumiwe na mataifa ya magharibi kuwa ndio silaha ya kuishurutisha Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran kuacha mpango wake wa nyuklia.

Marekani, Ufaransa na Uingereza ni miongoni mwa nchi zinazounga mkono vikwazo vipya dhidi ya Iran kwa ajili ya kuizuia nchi hiyo kutengeneza silaha za nyuklia.

Matamshi hayo ya China sasa yanaiweka nchi hiyo katika kambi moja na Urusi ambayo inapinga vikwazo dhidi ya Iran.

Wakati huo huo waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov anafanya ziara ya ghafla mjini Tehran kwa mazungumzo na rais Mahmoud Ahmednejad.

Lengo la ziara hiyo halikutangazwa licha ya kwamba waziri huyo wa mambo ya nje wa Urusi anafanya ziara hiyo wiki mbili tu baada ya rais Vladimir Puttin kukamilisha ziara yake nchini Iran.