1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING:Mazungumzo ya Korea Kaskazini yakwama tena

21 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCGm

Mazungumzo kuhusu mpango wa nuklia wa Korea Kaskazini yamekwama tena kufuatia kucheleweshwa kuhamishwa kwa fedha zilizozuiliwa na Marekani hadi benki moja ya Uchina.

Kikao hicho cha siku tatu kilichoanza siku ya jumatatu kililenga kujaribu kutekeleza makubaliano ya kufunga kiwanda cha nuklia cha Korea Kaskazini katika kipindi cha siku 60.Washiriki wengine wa mazungumzo kwa upande wao wanaahidi kutoa misaada ya nishati na kibinadamu endapo hayo yanatimizwa.

Korea Kaskazini inashikilia kuwa sharti ihamishiwe hela hizo kutoka Macau ndipo mazungumzo yaendelee.

Kulingana na mjumbe wa Korea Kusini Chun Yung-Woo juhudi zinaongezwa ili kuhamisha pesa hizo.Kulingana na Christopher Hill mjumbe wa Marekani,bado kuna imani kuwa mataifa sita wanachama ya Korea zote mbili,Marekani ,Uchina ,Japan na Urusi huenda wakatimiza makubaliano ya Februari. Korea Kaskazini ilisusia mazungumzo hayo ya oande sita kwa zaidi ya mwaka mmoja huku ikilaumu kuzuiliwa kwa fedha hizo baaada ya Marekani kulaumu Benki ya Macau iliyoweka fedha hizo kuficha shughuli za magendo za Korea Kaskazini.