1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING.Rais wa China ziarani Afrika

30 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCWa

China imesema kwamba itadhamini mazungumzo ya pande sita yanayolenga kutatua mzozo wa nyuklia wa Korea kaskazini.

Mazungumzo hayo yanatarajiwa kuanza tarehe 8 mwezi Februari.

Mazungumzo hayo yatazihusisha nchi za Korea kaskazini na Kusini, Marekani, China, Urusi na Japan na yanalenga kuishawishi Korea Kaskazini kuacha mpango wake wa nyuklia.

Lakini pamekuwepo na mafanikio madogo sana tangu mazungumzo hayo yalipoanza mwaka 2003.

Wakati huo huo kiongozi wa China Hu Jintao ameanza ziara yake katika nchi nane za Afrika.

Beijing inaazimia kujizatiti katika uhusiano wake wa kisiasa na kiuchumi na bara la Afrika.

Hii ni ziara ya tatu ya kiongozi wa China katika bara la Afrika tangu mwaka 2003.

Ziara ya siku 12 ya rais Hu Jintao itampeleka mpaka Sudan ambako anatarajiwa kuishinikiza Khartoum kutoa ushirikiano kwa Umoja wa mataifa katika juhudi za kumaliza ghasia katika jimbo la Darfur.

Kiongozi huyo wa China kwanza atazuru Cameroon katika ziara yake hiyo ya nchi nane za Afrika.