1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beirut. Aliyeuwawa katika maandamano azikwa.

5 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCmI

Maelfu ya waandamanaji wamelichukua jeneza la mtu mmoja Mshia ambaye aliuwawa wakati wa maandamano mjini Beirut , kwa mazishi leo Jumanne. Mamia ya wanajeshi wa ziada wamewekwa katika mji huo mkuu wa Lebanon baada ya mauaji hayo kuleta hali ya wasi wasi zaidi.

Upinzani unaoongozwa na chama kinachounga mkono Syria cha Hizboullah unailaumu serikali inayoungwa mkono na mataifa ya magharibi kwa kifo hicho cha mmoja kati ya waandamanaji baada ya maandamano yaliyokuwa ya amani siku ya Jumapili.

Wakati huo huo waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier amemtaka rais Assad wa Syria kulidhibiti kundi la Hizboullah nchini Lebanon ili lisiendelee kuleta madhara kwa jamii ya nchi hiyo.

Waziri mkuu wa Lebanon Fouad Siniora ameshutumu mauaji hayo na kuamuru uchunguzi ufanyike. Tangu siku ya Ijumaa , upande wa upinzani umekuwa ukifanya maandamano dhidi ya serikali ya Siniora katika juhudi za kuiangusha. Amekataa madai hayo na amepata uungwaji mkono wa serikali kadha za mataifa ya kiarabu na nchi za magharibi, ikiwa ni pamoja na Marekani, Uingereza, Ujerumani na Jordan.