1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT : Amri ya kutotembea yaondolewa

26 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCXj

Jeshi la Lebanon limeondowa amri ya kutotembea wakati wa usiku katika mji mkuu wa nchi hiyo Beirut kufuatia kuenea kwa vurumai katika chuo kikuu kati ya wanafunzi wanaoiunga mkono serikali na wake wanaoipinga kulikopelekea kuuwawa kwa watu wanne.

Ghasia hizo zilizojumuisha mapambano ya silaha kati ya mahasimu wa Kisunni na Kishia zimetia kiwingu mpango wa msaada wa euro bilioni sita ulioahidiwa kutolewa na wafadhili mjini Paris Ufaransa kwa ajili ya serikali ya Waziri Mkuu wa Lebanon Foad Siniora inayoungwa mkono na mataifa ya magharibi ambao ameuita kuwa ni kwa ajili ya wananchi wote wa Lebanon.

Mpango huo wa msaada unakusudia kuijenga upya Lebanon baada ya vita vya mwaka jana kati ya Israel na kundi la Hezbollah linaloungwa mkono na Syria.

Hali ya mvutano ilizidi kupamba moto nchini humo hapo Jumanne wakati wa mgomo wa taifa ulioongozwa na Hezbollah na washirika wake wa Kikristo.

Upinzani huo unataka kuitishwa kwa uchaguzi na mapema na kuundwa kwa serikali mpya.