1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beirut. Hizbolah waingia mitaani kuipinga serikali.

1 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCna

Maelfu ya Walebanon waliokuwa wakipepea bendera wamemiminika katika eneo la kati la Beirut kwa ajili ya maandamano yanayoongozwa na kundi la Hezboullah yenye lengo la kuiangusha serikali ya nchi hiyo inayoungwa mkono na mataifa ya magharibi.

Hezboullah inayoiunga mkono Syria pamoja na washirika wake wamewataka Walebanon nchini humo kushiriki katika maandamano , ambayo yatafuatiwa na tukio la kukaa karibu na ofisi za serikali. Hezboullah , ambayo inaungwa mkono na Syria na Iran , imeieleza serikali ya Lebanon kuwa ni kibaraka wa Marekani.

Waziri mkuu wa Lebanon Fouad Siniora ameapa kutoyumbishwa na maandamano hayo.