1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Jeshi la majini la Ujerumani lakabidhiwa usukani wa kulinda pwani ya Lebanon

16 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD2P

Jeshi la wanamaji kutoka Ujerumani limekabidhiwa ulinzi wa pwani ya Lebanon katika jukumu la kikosi cha Umoja wa mataifa cha kulinda amani nchini Lebanon, UNIFIL.

Sherehe zilifanyaka jana kwenye meli ya kijeshi ya kubebea ndege ya Italy,Garibaldi, ambayo imetia nanga kwenye bandari ya Beirut.

Wanajeshi wanamaji kutoka Ujerumani wameshika nafasi ya wanajeshi kutoka Italy na Ufaransa ambao walikuwa wakilinda pwani ya Lebanon chini ya makubaliano ya azimio la Umoja wa mataifa la kuvimaliza vita vya mwezi mzima kati ya Israeli na wapiganaji wa Hezebollah nchini Lebanon. Jukumu la wanajeshi hao kutoka Ujerumani ni kuhakikisha kwamba silaha haziingii na kusaidia jeshi la serikali ya Lebanon kulinda pwani na mipaka ya nchi.