1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Jeshi limetangaza amri ya kuzuia kutoka nje

26 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCXr

Nchini Lebanon,jeshi limetangaza amri ya kuwazuia watu kutoka nje katika mji mkuu, Beirut.Hatua hiyo imechukuliwa baada ya watu wasiopungua 3 kuawa na wengi wengine kujeruhiwa katika mapambano yaliozuka chuo kikuu cha Beirut,kati ya wafuasi wa serikali ya waziri mkuu Fouad Siniora na upande wa upinzani.Ghasia hizo zimetokea siku mbili baada ya watu watatu pia kuuawa na dazeni kadhaa kujeruhiwa katika mapambano yaliyozuka wakati wa mgomo mkuu nchini humo.Upinzani unaoongozwa na Hezbollah uliitisha mgomo huo katika jitihada ya kutaka kuiangusha serikali ya waziri mkuu Fouad Siniora.Siku ya Alkhamisi, Siniora alihudhuria mkutano wa wafadhila wa kimataifa mjini Paris,ambako Lebanon iliahidiwa msaada wa Dola bilioni 7.6.Pesa hizo zitasaidia kuijenga upya Lebanon,iliyoathirika vibaya wakati wa vita vya mwaka jana kati ya wanamgambo wa Hezbollah na Israel.