1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT : Maandamano dhidi ya serikali yaendelea

2 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCnM

Maandamano ya umma yanaendelea kwa siku ya pili katika mji mkuu wa Lebanon Beirut.

Wafuasi wa upinzani unaoongozwa na Hezbollah wanadai kujiuzulu kwa serikali ya Lebanon inayoungwa na mkono na mataifa ya magharibi inayoongozwa na Waziri Mkuu Fouad Siniora. Inakadiriwa kwamba watu waliojitokeza kwenye maandamano hayo hapo jana wanafikia 800,000 ambayo ni sawa na theluthi moja ya idadi ya watu nchini Lebanon.Maandamanao hayo yanaonyesha jinsi nchi hiyo ilivyogawika kwa misingi ya kikabila ambapo Washia wakiwaunga mkono Hezbollah na Wasunni walio wengi kwenye serikali wakimuunga mkono Siniora juu ya kwamba kundi la Wakriso pia linawaunga mkono Hezbollah.

Hezbollah inamshutumu Siniora kwa kuwa na mahusiano ya karibu mno na Marekani.

Siniora amesema serikali yake haitishiki na maandamano hayo.