1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Merkel akutana na Siniora

2 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCD1

Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel amesema Ujerumani inaunga mkono kuundwa kwa taifa la Lebanon litakalokuwa na uhuru. Merkel ameyasema hayo baada ya kukutana na waziri mkuu wa Lebanon, Fouad Siniora na spika wa bunge, Nabih Berri, mjini Beirut hii leo.

Kansela Merkel amewahimiza viongozi hao wamalize tofauti zao na kuutanzua mgogoro wa kisiasa ndani ya Lebanon.

Katika kumaliza ziara yake ya siku tatu ya Mashariki ya Kati kansela Merkel amekitembelea kikosi cha wanamaji wa Ujerumani walio sehemu ya jeshi la Umoja wa Mataifa la kulinda amani nchini Lebanon.