1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beirut. Mwanajeshi auwawa na wengine wajeruhiwa.

24 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBoz

Majeshi ya Lebanon yameshambulia kwa makombora kambi ya wakimbizi wa Kipalestina kaskazini ya nchi hiyo baada ya wapiganaji wanaohusiana na al-Qaeda kumpiga risasi na kumuua mwanajeshi mmoja na kuwajeruhi wengine watatu.

Duru za kiusalama zinasema kuwa wapiganaji wa Fatah al-Islam waliwashambulia wanajeshi hao wanne katika kambi ya Nahr al-Bared.

Makombora yalirushwa katika kambi hiyo ambako wapiganaji wapo baada ya kujiondoa kutoka katika maeneo ya wazi ambayo yamekamatwa na majeshi ya nchi hiyo.

Jeshi la Lebanon limedai kupata ushindi siku ya Alhamis baada ya siku 33 za mapigano dhidi ya wapiganaji hao wa Fatah al-Islam ambapo watu 172 wameuwawa.

Lakini jeshi hilo limesema kuwa halitaondoa hatua yake ya kuizingira kambi hiyo hadi pale wapiganaji hao wote watakapojisalimisha.