1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Operesheni kuwangóa wapiganaji wa Fatah al-Islam

22 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBpS

Majeshi ya Lebanon yanaendelea na operesheni yake ya kijeshi katika kambi ya wakimbizi wa Kipalestina ya Nahr al-Bared,kaskazini mwa nchi. Lengo la operesheni hiyo,ni kuwangóa wapiganaji wa kundi la Fatah al-Islam waliojificha katika kambi hiyo.Hapo awali,waziri wa ulinzi wa Lebanon alisema,wanamgambo waliojicha katika kambi hiyo ya wakimbizi wameshindwa na sasa majeshi yanashughulika na operesheni ya kuisafisha kambi. Ripoti zinasema,maelfu ya wakimbizi wa Kipalestina,wamebakia upande wa kusini wa kambi hiyo.Wanajeshi 76 wameuawa na 150 wengine wamejeruhiwa katika mapigano ya siku 33.