1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beirut. Solana aelekea katika ziara ya mashariki ya kati.

12 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCJq

Mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya Javier Solana amewasili mjini Beirut kwa mazungumzo na viongozi wa Lebanon.

Siku ya Jumanne Solana anakwenda Saudi Arabia kabla ya kuizuru Syria siku ya Jumatano. Umoja wa Ulaya unamatumaini kuwa ziara hiyo itasaidia kupunguza mzozo wa kisiasa nchini Lebanon na kuleta hali ya maridhiano zaidi kati ya makundi hasimu ya Wapalestina. Mahusiano rasmi kati ya umoja wa Ulaya na Syria yamesitishwa tangu pale waziri mkuu wa Lebanon Rafik Hariri alipouwawa kwa bomu February mwaka 2005. Shambulio hilo limehusishwa kwa kiasi fulani na utawala wa Damascus.