Beirut. Tanki la gesi lalipuka katika kampuni ya mikate.
24 Desemba 2006Matangazo
Mlipuko umetokea karibu na chuo kikuu cha Marekani mjini Beirut mapema leo, kituo cha televisheni cha Al-Jazeera kimeripoti, wakati polisi wa Lebanon wamesema mlipuko huo umetokea katika kampuni ya kuoka mikate.
Kwa mujibu wa duru za polisi nchini Lebanon , mlipuko huo , ama sauti ya mlipuko , ulitokea katika kampuni ya kuoka mikate karibu na viwanja vya chuo kikuu.
Polisi wamesema hakuna taarifa za kuumia kwa watu.