1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT : Uchaguzi wa rais umeahirishwa

22 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Dc

Uchaguzi wa rais nchini Lebanon umeahirishwa kwa takriban wiki tatu.

Spika wa bunge Nabih Berri amesema kwenye taarifa uchaguzi huo umeahirishwa kutoka Jumanne hadi tarehe 12 mwezi wa Novemba.Berri amesema uchaguzi huo umeahirishwa ili kutowa muda zaidi kwa makundi hasimu yanayounga mkono na yenye kuipinga Syria kukubaliana kwa kufikia muafaka juu ya mgombea wa wadhifa huo.

Bunge litamchaguwa rais mpya kuchukuwa nafasi ya Rais Emile Lahod anayeipendelea Syria ambaye muda wake unamalizika hapo tarehe 23 mwezi wa Novemba.