1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Vikosi vyapambana na wafuasi wa Fatah al-Islam

8 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBtq

Kwa mujibu wa duru za usalama nchini Lebanon, mwanajeshi mmoja ameuawa na wengine watatu wamejeruhiwa katika mapigano yaliyozuka na kundi la Fatah al Islam,kwenye kambi ya Nahr al Bared, karibu na mji wa Tripoli.Katika shambulizi jingine,kaskazini mwa mji mkuu Beirut,bomu liliripuka katika eneo la viwanda ambako Wakristo wengi huishi.Raia mmoja aliuawa na wanne walijeruhiwa katika mripuko huo wa bomu.Jumla ya watu 115 wameuawa,tangu kuzuka kwa mapigano,kati ya wanamgambo na vikosi vya serikali hapo tarehe 20 mwezi Mei.