1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT : Wanajeshi watano wauwawa katika mapambano

10 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBtC

Wanajeshi watano wa Lebanon wameuwawa katika mapambano mapya na wanamgambo wanaochochewa na kundi la Al Qaeda waliojichimbia kwenye kambi ya wakimbizi wa Kipalestina.

Vikosi vya usalama vimesema wanajeshi wengine 21 wa Lebanon wamejeruhiwa katika mapambano ndani na karibu na kambi hiyo ya wakimbizi ya Nahr al Bared ilioko kaskazini mwa mwa mji wa Tripoli.

Tokea kuzuka kwa mapigano kati ya wanamgambo hao na jeshi la Lebanon wiki tatu zilizopita zaidi ya watu 100 wameuwawa wakiwemo wanajeshi 50.