1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT:Hezebollah na Israeli wazungumzia juu ya hatima ya wafungwa

1 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCx8

Kiongozi wa kundi la Hezebollah nchini Lebanon, Sayyed Hassan Nasrallah, amesema mazungumzo kati ya kundi lake na Israel yameanza juu ya kubadilishana wafungwa wakisaidiwa na mpatanishi wa Umoja wa mataifa. Akizungumza kwenye televisheni inaomilikiwa na Hezebollah, Nasrallah amesema ´´mazungumzo ya kuaminika yamekuwa yakiendelea chini ya upatanishi wa mjumbe wa kisiri wa Umoja wa mataifa´´.

Kundi la Hezebollah liliwakamata wanajeshi wawili wa Israeli katika shambulio kwenye mpaka tarehe 12 Julai mwaka huu na kuzusha mashambulizi ya ndege za kivita za Israeli kwa muda wa siku 34. Israeli haijasema lolote juu ya matamshi ya kiongozi wa kundi la Hezebollah, Hassan Nasrallah.