1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUTI:Kansela Merkel ahitimisha ziara Mashariki ya Kati ndani ya meli

3 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCCp

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amehitimisha ziara yake katika Mashariki ya Kati kwa kutembelea meli ya kivita ya Ujerumani iliyoko kwenye pwani ya Lebanon.

Ujerumani ina askari 1600 katika jeshi la Umoja wa Mataifa linalofanya doria katika pwani hiyo ya Lebanon.

Kansela Merkel aliwapongeza askari hao ambao kwa kushirikiana na wengine walifanikiwa kumaliza vita ya mwezi mwaka jana kati ya Israel na wanamgambo wa Hizbollah.

Mapema katika mazungumzo yake na Waziri Mkuu wa Lebanon, Kansela Merkel alisisita haja ya Lebanon kuwa huru zaidi.

Pia aliitaka Syria kutoa ushirikiano mkubwa kwa tume ya Umoja wa Mataifa inayochunguza kifo cha Waziri Mkuu wa zamani wa Lebanon Rafik Harir miaka miwili iliyopita.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Lebanon Fuad Siniora alimshukuru Kansela Merkel.