1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beirut.Malaki ya watu wajitokeza kuusindikiza mwili wa Pierre Gamael.

23 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCq0

Umati wa watu zaidi ya laki mbili, wamehudhuria mazishi ya Waziri wa Viwanda Pierre Gamayel katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut.

Watu hao walikuwa wakipeperusha bendera ya Taifa na za chama cha Wafalanji-Wakiristo wa Lebanon.

Kiongozi wa kanisa Katoliki Ulimwenguni Papa Benedict wa 16 amelaani mauaji hayo na kuwatolea mwito Walebanon wawe na umoja.

Mkuu wa jamii ya madhehebu ya Druz, Walid Jumlat akihutubia katika mazishi hayo amemtaja Pierre Gemayel kua ni ”Shahidi katika kuwania haki”.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan amesema.

”Nimewatolea mwito viongozi wa eneo hilo, ikiwa ni pamoja na Syria na Iran, washirikiane na pande zote ili kudhamini umoja na utulivu nchini Lebanon na kuhimiza subira kwa pande zote”

baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeitaka Korti kuu ya Kimataifa ichunguze kisa cha kuuliwa Pierre Gemayel, sawa na ilivyofanya kuhusiana na kuuliwa Waziri Mkuu wa zamani wa Lebanon Rafik Hariri.