1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT:Maombolezo zaidi ya mauaji ya mbunge

20 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBO7

Ofisi za serikali, mabenki pamoja na shule vimefungwa nchini Lebano mnamo wakati huu ambapo nchi hiyo inaombeleza mauaji ya mbunge ambaye alikuwa mpinzani mkubwa wa Syria.

Mbunge huyo Antoine Ghanim kutoka Chama cha Maronite Phalange aliuawa kwa bomu pamoja na watu wengine sita katika kitongoji kinachokaliwa na wakristo mjini Beirut.

Wizara ya Elimu nchini humo imesema kuwa shule zote pamoja na vyuo vikuu vitaendelea kufungwa mpaka kumalizika kwa mazishi ya mbunge huyo hapo kesho.

Waziri Mkuu wa Lebanon Fuad Siniora amesema uchaguzi mkuu uliyopangwa kufanyika wiki ijayo utaendelea kama ulivyopangwa na ameuomba Umoja wa Mataifa kufanya uchunguzi juu ya mauaji hayo.