1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT.Mawaziri 18 waidhinisha mswaada wa kuundwa mahakama maalum

13 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCt6

Baraza la mawaziri la Lebanon limeuidhinisha mswaada uliodhaminiwa na umoja wa mataifa wa kuundwa mahakama maalum itakayo sikiliza kesi ya mauaji ya aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon Rafik Hariri.

Saad Hariri kiongozi wa kundi linalopinga sera za Syria nchini Lebanon amesema.

Oton……Utawala wa Syria unawajibika kwa mauaji ya Rafik Hariri na wengine wote. Kwa nini kuwahifadhi wauwaji wa raia wa Leabnon, watu wa Lebanon, viongozi, viongozi wa kidini ,waandishi wa habari na wabunge..sielewi lakini kwa hilo lazima waamke.

Mawaziri 18 pekee ndio waliokutana kupitisha azimio hilo baada ya jumla ya mawaziri 6 kujiuzulu kutoka serikalini. Waziri wa mazingira Yacoob Sarraf ndio waziri wa sita kujiuzulu baada ya mawaziri wenzake watano kujiuzulu siku ya jumamosi. Sarraf amesema kuwa amejiuzulu kwa kuwa serikali ya waziri mkuu Fouad Siniora si halali tena.

Waziri mkuu wa Lebanon Fouad Siniora anae elemea upande unaopinga sera za Syria wenye wafuasi wengi bungeni amekataa kukubali pendekezo la kujiuzulu kwa mawaziri hao.

Rais Emile Lahoud anaeungwa mkono na Syria amemuandikia barua waziri mkuu Siniora kwamba serikali yake si halali.