1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beirut:Uchunguzi wa kifo cha Pierre Gamayel waanza.

24 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCpn

Uchunguzi wa kimataifa umeanza mjini Beirut kujua nani walikua nyuma ya kuuliwa waziri wa viwanda wa Libnan-Pierre Gemayel.Wachunguzi wa kimataifa wameanza mazungumzo pamoja na maafisa wa ngazi ya juu wa idara ya sheria mjini Beirut.

Tume hiyo ya uchunguzi imeundwa na Umoja wa mataifa.Jana maelfu ya watu walihudhuria maziko ya Pierre Gemayel mjini Beirut.

Jeneza la mwanasiasa huyo kijana lilizungushwa katika mitaa ya Beirut huku bendera za Libnan zikipepea.

Waandamani walikua wakipaza sauti kuilaani Syria na washirika wake nchini Libnan kua nyuma ya mauwaji nchini Libnan.

Naibu waziri wa mambo ya nchi za nje wa Syria,FAYSAL MEKDAD anasema:

„Huu ni uhalifu wa kweli uliolengwa,namaanisha ikiwa tunataka kuzungumza kisiasa,uliolengwa kubadilisha wezani wa nguvu nchini Libnan,kishindo ambacho baadhi ya watu nchini Libnan wanakabiliana nacho kutokana na umaarufu wa Syria miongoni mwa wengi kati ya wananchi wa Libnan.

Tunataka uchunguzi ufanywe kujua nani walikua nyuma ya mauwaji haya na tunaamini siku itafika ambapo ukweli utajulikana na kujulikana pia wanaouwa watu nchini Libnan.Na bila ya shaka haitakua Syria.“