1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT.Ujerumani yatwaa hatamu za kuongoza kikosi cha kulinda amani nchini Lebanon

16 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD2I

Kikosi cha wanamaji wa Ujerumani kimeanza rasmi hatamu za kuongoza shughuli za kuweka doria nchini Lebanon chini ya mpango wa kulinda amani wa umoja wa mataifa tangu kutiwa saini makubaliano ya kusimamisha vita kati ya majeshi ya israel na wapiganajni wa Hezbollah nchini Lebanon.

Manowari nane za kikosi cha majini cha Ujerumani zimetia nanga katika pwani ya Lebanon.

Jumla ya wanamaji 1000 wakiwemo wanamaji kutoka Denmark, Norway, Netherland na Sweden watweka doria kuzuia kuingizwa silaha kinyume cha sheria kwa wapiganaji wa Hezbollah.

Waziri wa mambo ya nje wa Uhispania Miguel Angel Moratinos aliyezuru Damascus mwishoni mwa wiki amesema kuwa Syria imetekeleza uamuzi wa baraza la usalama la umoja wa mataifa namba 1701 kwa kukubali kushiriki katika kupunguza hali ya mvutano ianyoleta wasiwasi.