1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT:Umoja wa Ulaya na harakati za kuikoa hali ya kisiasa Lebanon

20 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7E9

Mawaziri wa mambo ya nje wa Ufaransa,Italia na Uhispania wanakutana na viongozi wa Lebanon hii leo kujadili mzozo wa kisiasa unoendelea unaotishia kuzuia uchaguzi wa rais nchini humo.

Bernad Kouchner,Massimo D’alema na Miguel Angel Moratinos wanakutana na waziri mkuu Fuad Siniora spika wa bunge Nabih Berri na kadinali Nasralla Sfeir kiongozi mwenye usemi mkubwa katika jamii ya wakristo nchini Lebanon.Mkutano huo unalengo la kujaribu kumaliza mivutano ya kisiasa inayosababisha kuzuia bunge lisifanye uchaguzi war ais atakayochukua mahala par ais anayeegemea Syria Emile Lahoud anayemaliza muda wake madarakani Novemba 24.

Hata hivyo vyombo vya habari vya Lebanon vimeripoti kwamba ziara hiyo ya siku moja ya viongozi hao wa nchi za magharibi haitafua dafu katika kurekebisha hali ya kisiasa nchini humo kwa sababu tayari imearifiwa kikao cha kumchagua rais kinatarajiwa kukhairishwa.Serikali ya waziri mkuu Siniora imelemazwa tangu upinzani ulipowandoa mawaziri wake sita katika serikali mwezi Novemba mwaka 2006 katika juhudi za kutaka kuwakilishwa zaidi serikalini.