1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIT HANOUN: Israel inaendelea na mashambulio katika Gaza

2 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCwf

Mashambulio ya vikosi vya Israel katika mji wa Beit Hanoun yanaendelea.Operesheni hiyo ya kijeshi ni kubwa kabisa kupata kufanywa na Israel katika Ukanda wa Gaza tangu miezi kadhaa.Msemaji wa wizara ya kigeni ya Israel,Mark Regev amesema, vikosi viliingia mji huo siku ya Jumatano kwa azma ya kuteketeza vituo vinavyotumiwa na wanamgambo kuirushia Israel makombora.Kwa mujibu wa maafisa wa matibabu,mapamabano ya hii leo yameua Wapalestina 4.Hadi Wapalestina 9 na mwanajeshi mmoja wa Kiisrael waliuawa katika mapambano jana.