1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bekele, Jeptoo kushiriki mbio za Chicago marathon

5 Septemba 2014

Bingwa anayeshikilia rekodi ya ulimwengu Muethiopia Kenenisa Bekele na bingwa mtetezi Mkenya Rita Jeptoo ni miongoni mwa waliothibitishwa kushiriki mbio za Chicago marathon mwezi ujao.

https://p.dw.com/p/1D7kO
Äthiopien Kenenisa Bekele
Picha: picture-alliance/dpa

Mkenya Dennis Kimetto, mshindi wa Chicago marathon mwaka jana kwa upande wa wanaume aliamua kushiriki katika mbio za mwezi huu za Berlin marathon badala ya kutetea taji lake la barabara za Chicago mnamo Oktoba 12.

Lakini jukwaa liko tayari kwa kinyang'anyiro kikali wakati Muethipia Bekele, anayeshikilia rekodi ya ulimwengu katika mbio za mita 10,000 na 5,000 na aliyejitokeza katika ulimwengu wa marathon mwaka huu, akikabiliwa na hasimu wake Mkenya Eliud Kipchoge, mwanariadha wa masafa marefu aliyejipa jina katika mbio za Hamburg marathon mwaka jana.

Bekele alishinda mbio zake za wkanza za marathon mwezi Aprili mwkaa jana mjini Paris kwa kutumia mud awa saa 2:05:04. Nyota wengine watakaoshiriki Chicago marathon kwa wanaume ni wakenya Sammy Kitwara, Bernard Koech na Dickson Chumba. Na kwa upande wa wanawake miongoni mwa washindani wa Jeptoo watakuwa ni Jemima Sumgong, Florence Kiplagat wote wa kutoka Kenya na MuEthiopia Birhane Dibaba

Mwandishi:Bruce Amani/AFP/DPA/reueters
Mhariri:Josephat Charo