1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BELGRADE: Raia wa Serbia wapiga kura kwenye uchaguzi mkuu.

21 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZ4

Raia wa Serbia wanapiga kura leo kwenye uchaguzi mkuu.

Vyama ishirini, baadhi vikiwa na misimamo ya kitaifa na vingine vikiunga mkono siasa za kimagharibi, vinawania viti mia mbili vya bunge.

Uchunguzi wa hivi karibuni umeonyesha chama cha Serbian Radical Party kinachozingatia utaifa kitakabiliana vikali na chama cha Democratic kinachoungwa mkono na mataifa ya magharibi.

Uchaguzi huo unaandaliwa siku kadhaa kabla ya mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuwasilisha mpango wake kuhusu jimbo la Kosovo ambalo limekuwa likismamiwa na Umoja huo tangu mwaka elfu moja mia tisa na tisini na tisa.