1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BELGRADE: Suala la Kosovo bado linazua mzozo

3 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCVf

Viongozi wa Waserbia na Waalbania hawajaelewana bado kuhusu mustakabali wa jimbo la Kosovo baada ya mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa, Martti Ahtisaari, kutoa muswada wa mapendekezo kuhusu hatma ya jimbo hilo.

Viongozi wa Waalbania walio wengi, wameunga mkono mpango huo ambao unapendekeza jimbo la Kosovo liandaliwe taratibu za kuelekea kujitawala kwa usimamizi wa Umoja wa Mataifa.

Hata hivyo Rais wa Serbia, Boris Tadic amepinga muswada huo akisema serikali yake haitaruhusu kamwe jimbo hilo kupewa uhuru.

Kosovo imekuwa ikisimamiwa na Umoja wa Mataifa tangu mwaka elfu moja mia tisa na tisini na tisa wakati majeshi ya NATO yalipoingilia kati na kumaliza vita kati ya serikali ya Yugoslavia na wapiganaji wa Kialbania.