1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BELGRADE: Wito kususia chaguzi za Kosovo

13 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBQ4

Serbia imetoa mwito kwa Waserb wa Kosovo kutoshiriki katika chaguzi za bunge na mabaraza ya mitaa zitakazofanywa katika jimbo la Kosovo. Taarifa iliyotolewa na serikali ya Waziri Mkuu Vojislav Kostunica imesema,serikali ya Serbia inaamini kuwa tangu ujumbe wa Umoja wa Mataifa kusimamia jimbo la Kosovo miaka minane iliyopita, Waserbia hawakuhakikishiwa hali za kimsingi za kuwapa maisha huru na ya usalama.

Chaguzi za Kosovo zimepengwa kufanywa Novemba 17.Tangu majeshi ya Belgrade kutimuliwa na vikosi vya NATO katika mwaka 1999 ili kukomesha ukandamizaji wa Waalbania walio wengi,Waserbia wanaishi katika maeneo yanayolindwa.Vile vile maelfu wengine wameondoka Kosovo wakihofia mashambulizi ya kulipiza kisasi.