1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bellingham atulia vyema Madrid

28 Agosti 2023

Mchezaji wa zamani wa Borussia Dortmund Jude Bellingham ambaye alijiunga na Real Madrid anaendelea kuonyesha cheche zake kwani katika mechi yake ya tatu ya La Liga amefunga goli lake la 4.

https://p.dw.com/p/4Vevx
Uhispania | Jude Bellingham akitambulishwa kwa Real Madrid
mchezaji wa Real Madrid Jude BellinghamPicha: Isabel Infantes/empics/picture alliance

Goli hilo alilofunga Bellingham katika mechi ya Madrid dhidi ya Celta Vigo, lilitosha kuwapa pointi zote tatu na kuwapa ushindi wa tatu mfululizo katika ligi.

Ni wachezaji wengine sita pekeyao waliofunga katika mechi tatu za kwanza za La Liga wakiichezea Real Madrid.

Orodha hiyo inawajumuisha wakongwe wa klabu hiyo kama Cristiano Ronaldo, Jorge Valdano na Hugo Sanchez.

Vyanzo: Reuters/DPAE